22 NOVEMBA 2024
Manage episode 451561911 series 2027789
内容由UN Global Communications (Digital Solutions Unit) and United Nations提供。所有播客内容(包括剧集、图形和播客描述)均由 UN Global Communications (Digital Solutions Unit) and United Nations 或其播客平台合作伙伴直接上传和提供。如果您认为有人在未经您许可的情况下使用您的受版权保护的作品,您可以按照此处概述的流程进行操作https://zh.player.fm/legal。
Hii leo jaridani tunaangazia majadiliano huko Baku Azerbaijan kuhusu ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi, na kazi za walinda amani kutoka Tanzania TANZBATT-11 huko DRC. Makala inaturejesha kataika mkutano wa COP29 na mashinani inatupeleka Namibia, kulikoni?Majadiliano ya mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 yamekumbwa na mkwamo huko Baku Azerbaijana muafaka haujapatikana. Majadiliano hayo yaliyotarajiwa kukunja jamvi leo sasa yanaendelea kwa kuwekwa mezani mapendekezo mapya kuhusu ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi hasa kwa matifa yanayoendelea.Umoja wa Mataifa unasema kwamba vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imefanya taifa hilo kuwa pahala hatari zaidi duniani kwa watoto kuishi, kutokana na mateso ya kimwili na kisaikolojia wanayoyapitia. Kwa kutambua hilo walinda amani wanawake wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye ujumbe wa UN nchini humo, MONUSCO wamechukua hatua kuona watoto wanaishi kama watoto.Makala inakupeleka Baku nchini Azerbaijan kunakotamatika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 kumsikia kijana kutoka Tanzania akizungumzia kilichompeleka, anachoondoka nacho na ujumbe wake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.Na katika mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP, tunasikia kauli ya Willem Westhuizen, mkulima kutoka Namibia, akielezea changamoto zinazotokana na ukame unaoathiri maisha yao kila siku”. Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu!
…
continue reading
100集单集